UNABII WA HABARI ZA BIBLIA: Jan-March 2014
Ndani ya toleo hili:
3 Wakristo Wameifundisha Injili ya Ufalme! Je, Wakristo wa karne ya kwanza na ya pili walikuwa wanaelewa na walihubiri juu ya Ufalme wa Mungu? Vipi kuhusu Wakristo wa karne ya 20 na ya 21?
8 Miezi ya Rangi kama Damu: Je, Yesu Atarejea 2014? “Miezi ya Rangi kama Damu”
inatarajiwa kutokea katika mwaka 2014. Je, hali hiyo yaweza kuwa inaashiria kwamba Yesu atarejea mwaka 2014?
15 Jisomee Kozi ya Biblia Somo la 1: Kwa nini Tujifunze Biblia? Hili ndilo somo la kwanza la Kozi ya kuwasaidia watu kuielewa Biblia.
27 Mardi Gras: Ni Sherehe ya Ibilisi? Mardi Gras; ambayo ni sikukuu ambapo watu siku hiyo huvaa mapambo na vinyago vya kutisha usoni yaonekana kuongezeka umaarufu. Baadhi wanaamini kwamba ni sherehe sahiihi hata kwa Wakristo. Lakini hili ni sawa?
32 Yesu Alimaanisha Nini – “Nataka Rehema, Wala si Sadaka”? Kulingana na Yesu, rehema ni moja ya mambo yaliyo “mambo makuu ya sheria” (Mathayo 23:23). Hapa tunakuletea makala iliyoandikwa kwenye gazeti la zamani la Good News, ifafanuayo juu ya hili.